Liverpool wapewa Atalanta robo fainali Europa
LIVERPOOL itacheza na Atalanta katika robo fainali ya Europa huku West Ham ikipangwa kumenyana na Bayer Leverkusen.
‘The Reds’ ambao wapo kwenye mashindano ya EPL, Europa, FA bado wana uwezo wa kutwaa mataji katika msimu wa mwisho wa Jurgen Klopp.
Wapinzani wa Italia, AC Milan na Roma wanakutana kugombea nusu fainali, huku klabu ya Benfica ya Ureno ikimenyana na Marseille ya Ligue 1.
Raundi ya kwanza itafanyika Aprili, 11 na Aprili 18 raundi ya pili.