Lori lauwa wawili kwa moto Morogoro

WATU wawili wamefariki dunia kwa kuungua moto kufuatia ajali ya lori lililobeba matufa kugongana uso kwa uso na lori la mizigo katika eneo milima ya Mikumi katika Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro kwenye barabara kuu ya Morogoro – Iringa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro ajali hiyo imetokea leo saa 3 asubuhi.

Advertisement

Ajali hiyo ilisababisha magari mengine yaliyokuwa yakitokea upande Iringa na Morogoro kusimama kwa muda. Baada ya shughuli za uokozi, magari yaliruhusiwa kuendelea na safari.