“Lowassa ilikuwa akitaka lake linakuwa”

Simanzi imetawala viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam, ambako mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, hayati Erward Lowassa unaagwa, huku waombolezaji mbalimbali wakitaja sifa zake.

Miongoni mwa waliopata fursa ya kuzungumza ni Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye aliyemuelezea hayati Lowassa kuwa ni kiongozi ambaye wakati wa uhai wake alisimamia kile alichokiamini na kwamba akitaka jambo lake liwe basi litakuwa.

“Edward Lowasa alikuwa akitaka jambo lake lazima liwe tunasherehekea maisha yake kwa busara zake ambazo alizionesha katika uongozi wake,” amesema Sumaye.

Viongozi mbalimbali wanaendelea kuzungumza katika tukio hilo la kuaga mwili wa hayati Lowasa.

Habari Zifananazo

Back to top button