Ludimo ajitosa Uenyekiti CCM Mwanza
MWANZA; Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Nyamagana, Comred Yusuph Ludimo ni miongoni mwa makada wa chama hicho waliojitokeza kuchukua, kurejesha na kushiriki katika usaili wa nafasi ya Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Sixbert Jichabu kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
Yusuph Ludimo aliwahi kuwa Katibu wa kwanza wa Shirikisho la Vyuo Vikuu (SENETI) Mkoa wa Mwanza, Katibu wa CCM tawi la Kambarage chuo Kikuu cha SAUT Mwanza, kaimu Katibu wa uhamasishaji na chipukizi UVCCM Mkoa wa Mwanza, mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa, mgombea wa nafasi ya mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Nyamagana 2017 nk.
Makada wengine waliojitokeza katika kinyang’anyiro hicho ni pamoja na Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mkoa wa Mwanza, Dk.
Antony Dialo, Nelson Mesha aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilemela, Chacha Boroi, Mjumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Mwanza John Nzilanyingi, Mjumbe wa kamati ya siasa, Elizabeth Nyingi, Mwenyekiti wa sasa wa CCM Wilaya ya Misungwi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ukerewe, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sengerema na wengineo.
Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza kilitangaza zoezi la kuchukua fomu kuanzia Novemba 12 hadi 16 .
2023 ambapo mchakato wa uchaguzi kwaajili ya kujaza nafasi wazi ya Mwenyekiti wa CCM mkoani humo utaendelea kwa vikao vya taifa kupitia mapendekezo ya ngazi ya mkoa, kujadili na kisha kurejesha majina ya wagombea kwaajili ya kuanza kampeni na kupigiwa kura na wajumbe kupata Mwenyekiti mteule.