M23 wavamia Kalembe

CONGO : WAASI wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wameuteka mji unaozozaniwa wa Kalembe, mashariki mwa Kongo, katika kile kilichotajwa kuwa hatua mpya ya ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha vita yaliyosainiwa Agosti mwaka huu.

Waasi hao waliingia katika mji wa Kalembe baada ya mapigano makali na kundi la wapiganaji wanaoungwa mkono na jeshi la Kongo.

Naye Msemaji wa kundi la wapiganaji wa jeshi la Kongo, Marcellin Shenkuku amesema  pamoja na waasi wa M23 kutwaa na kudhibiti moja ya maeneo yao, bado ni vigumu kusema ni nani anaudhibiti mji wa Kalembe kwa sasa.

Advertisement

SOMA: DRC Congo na Rwanda kumaliza mapigano