Maaskofu waungana kuwaombea viongozi, uchaguzi mkuu

MAASKOFU na wachungaji wa Makanisa ya Pentecoste wameungana na Msama Promotion kushiriki kuwaombea viongozi wa taifa na Uchaguzi Mkuu katika tamasha litakaloanza Juni 21, Dar es Salaam na kuelekea mikoa mingine.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili 13, Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama amesema viongozi hao wanashirikiana kuliombea tamasha liweze kufanikiwa.

“Tumefanya kikao na baadhi ya watumishi wa Mungu wakiwemo Maaskofu, wachungaji na mitume na tutaendelea kushirikiana nao kuhakikisha tamasha linafanikiwa,”amesema.

Advertisement

Amesema bado wanaendelea kuomba eneo la kufanyia tamasha hilo lakini wanasubiri kuona ombi lao la kutumia Uwanja wa Mkapa au Uhuru. Pia, wanaendelea kuzungumza na waimbaji wa muziki wa injili kutoka Afrika Kusini, Nigeria, Rwanda, Zambia na mataifa mengine wameshakubaliana nao. Kuhusu waimbaji wa ndani wameshamalizana nao.

Msama amesema anaendelea kufanya mazungumzo na wadhamini mbalimbali kwani kuwaleta wasanii wa kimataifa ni gharama kubwa wanahitaji watu wa kuwashika mkono ili kufika katika mikoa yote kama ilivyokusudiwa.

Kwa upande wake Askofu wa Makanisa ya Pentecoste Tegeta Ndesario Mlaki amesema wakati wanaingia kwenye uchaguzi wanahitaji amani na utulivu, wanamuunga mkono Msama katika maombi.

Filipo Mdara, mchungaji kiongozi Kanisa la FPCT Gongo la Mboto, amesema uchaguzi bila maombi hawawezi kufika kule wanakohitaji na kumshukuru Msama kwa kushirikiana kwa Umoja kuombea taifa.

Mchungaji Mika Fonka ambaye ni kiongozi wa Makanisa ya Pentecoste Wilaya ya Ilala alisema Taifa lolote likikosa maombi amani haiwezi kuwepo hivyo Kanisa lina jukumu la kuombea taifa.

Mchungaji Rose David wa Kanisa la Saa za ukombozi alisema: “tuungane katika kuombea uchaguzi tunaamini utafanikiwa, na kwa Umoja Wetu tutafanikiwa njooni kwa wingi siku hiyo,”

5 comments
  1. Hey this iis kind oof off tooic but I was wondeing iff blog use
    WYSIWYG edfitors or iif yyou hqve to manually code wkth HTML.
    I’m startng a blog sokon buut hafe nno coding exoerience
    so I wanted tto gett guidanche frrom someohe wifh experience.
    Anyy help would bbe enormously appreciated!

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *