SHIRIKA la Omuka Hub kwa kushirikiana na Shirika la FES Tanzania kupitia mkurugenzi wake, Neema Lugangira wameandaa semina ya sheria za uchaguzi na vyama vya siasa, kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa na ushiriki wa wanawake katika siasa kwa mabalozi wa CCM 227 wa Bukoba Mjini.
Semina hiyo ililenga kutoa mwongozo na kuongeza uelewa kwa mabalozi hao juu ya jamii hasa wanawake kushiriki moja moja katika kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotajarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu
Rugangira aliwahakikishia mabalozi hao kuwa Chama Cha Mapinduzi kupitia viongozi wake wote kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa wamewezesha kumsimamia vyema Ilani ya Uchaguzi na wananchi wamepata maendeleo makubwa kupitia Ilani ambayo imetekelezea hivyo nguvu kubwa ni kuhakikisha Kila mwenye haki ya kupiga kura anafika kituoni mapema kupiga kura.
“Mabalozi wa CCM ni jeshi kubwa moja ya lengo la semina hii ni kuona namna mnavyoweza kufikia jamii yote na kuendeleza ushawishi wa kuhakikisha wananchi wote bila kuwaacha wanawake katika kupiga kura na kuwapata viongozi shupavu ambao wataendelea kumsimamia Ilani ya chama ,na kumsimamia serikali kutekeleza miradi,” amesema Rugangira.
Pamoja na mada zingine, Katibu wa CCM Bukoba Mjini, Shabani Mdoe na Hadija Mkelenga Katibu wa UWT Bukoba Mjini waliwasilisha mada juu ya umuhimu wa wananchi kushiriki uchaguzi ,umuhimu wa wanawake kuchagua na kuchaguliwa katika jamii na wajibu wa mabalozi hao katika kuitumikia jamii na kumsimamia utekelezaji wa chama hicho.
Aidha, wakati wa Semina hiyo,Issa Gavu, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) – Oganaizesheni aliongea moja kwa moja na Mabalozi wa CCM 227 wa Bukoba Mjini kupitia simu ya Mbunge Lugangira na kujibu hoja zao na kupokea Salaam za Rais Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Mabalozi wa CCM wa Bukoba Mjini.
Gavu alipokea Shukrani za mabalozi kwa Rais wao na changamoto zao ambapo alitambua mchango mkubwa wa kazi zinazofanywa na mabalozi hao katika jamii.
Kauli mbiu katika mafunzo hayo ya mabalozi ilikuwa ni #KuraYanguFyuchaYangu