Mabondia JKT waahidi ushindi

MABONDIA wanawake kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wameahidi kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwenye pambano la wanawake  Machi 11, 2023 ukumbi wa Ubungo Plaza Dar es salaam.

Wakizungumza wakati wa maandalizi yao Mbweni JKT Dar es Salaam, Grace Mwakamele na Zawadi Wakutaka,  wamesema wapo tayari kuonesha ufundi wa ngumi, huku wakitamba kuibuka na ushindi dhidi ya wapinzani wao kutoka Zambia na Malawi.

Naye Mlezi wa mabondia kutoka Mbweni JKT Boxing Klabu, Mohammed Ramadan  amesema ana imani na mabondia hao kutokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya na kuahidi ushindi wa mapema.

Grace Mwakamele anatarajia kuzichapa na Lucia Ally kutoka Zambia,  huku Zawadi akizichapa na Mphatso Metauzu wa Malawi.

Habari Zifananazo

Back to top button