Madaktari waeleza umuhimu bima ya afya

CHAMA cha Madaktari Tanzania (MAT) kimesema mpango wa Bima ya Afya kwa Wote ni muhimu kwa kuwa utawasaidia wananchi kupata huduma bora ya afya kwa wakati na kuwaondolea mzigo wa kulipa gharama za matibabu.

Akizungumza wakati akihojiwa katika kipindi cha  Mizani kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Rais wa MAT, Dk Mugisha Nkoronko amesema amesema mpango huo utawasaidia wananchi kuepuka usumbufu wakiugua ghafla na utawarahisishia kupata huduma ya matibabu ya uhakika hata kama hawana fedha. “Bima ya Afya kwa Wote si mradi tu wa Wizara ya Afya bali ni mkataba wa ulinzi wa kitaifa kwani mpango huu umekuja kwa ajili ya kuwajali wananchi ili kuwasaidia katika kuimarisha afya zao,” alisema Dk Nkoronko.

Amesema Bima ya Afya kwa Wote itaisaidia serikali kuondoa mzigo wa kusamehe madeni ya wagonjwa wasiokuwa na uwezo. “Itaboresha afya na ustawi wa jamii na tutachangia nguvu kazi katika utafutaji kwa sababu bima itapunguza muda wa watu kukaa sana hospitali,” alisema Dk Nkoronko. SOMA: Bima ya Afya kwa Wote kutibu figo, moyo

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button