“Madini kichocheo kikubwa ukuaji uchumi”

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema sekta ya  madini ni kichocheo kikubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kuwa kijiji cha Mundarara kimekuwa na uzalishaji wa madini

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mundarara, Dk Biteko amesema  madini hayo kichocheo kikubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kuwa kijiji cha Mundarara kimekuwa na uzalishaji wa madini ya rubi yanayonufaisha jamii mbalimbali.

Ambapo amesema katika vijiji hivyo  52 vilivyopo wilaya ni hapo vina umeme, ambapo vitongoji 112 kati ya 176 vitongoji vyenye umeme ni 112 pekee lakini bado  maeneo ambayo yanahitaji nguzo 25 na amemuelekeza Meneja wa Tanesco ndani ya wiki tatu nguzo ziwekwe na watu wapate umeme.

Wakati huo Mmiliki wa kampuni ya Sendeu Agrovet Co. Ltd  na mwekezaji mzawa Gabriel Sendeu ametoa madawati 300 kwaajili ya shule tano za kata ya mundarara katika kurudisha faida kwa jamii kwani kupitia sekta hiyo wamenufaika nayo huku akiomba kituo cha cha afya katika kata hiyo kwaaajili ya wachimbaji madini na wananchi kupata huduma bora za afya karibu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button