MKALAMA, Singida: BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama limepitisha bajeti pendekezwa kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Akizungumza katika baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, James Mkwega ameipongeza Halmashauri sambasamba na kuwataka watumishi kusimamia vizuri bajeti hiyo kama ilivyopangwa katika kuleta maendeleo kwa wananchi na Wilaya kwa ujumla.
“Kwanza nawapongeza sana kwa bajeti nzuri. Nawaombeni sana, chondechonde nendeni mkasimamie bajeti vizuri. Tuna imani kubwa sana na serikali,” amesema Mkwega.
Awali akiwasilisha mapendekezo ya hayo, Mkurugenzi Mtendaji, Asia Messos amesema kwa mwaka wa fedha 2024/25, Halmashauri imepanga kukusanya na kutumia jumla ya Sh 29,966,375,000
“Kwa mwaka wa fedha 2024/25 Halmashauri ya wilaya Mkalama imepanga kukukusanya na kutumia jumla ya Sh 29,966,375,000 kwa ajili ya mishahara, matumizi mengineyo na miradi ya maendeleo.” Amesema Messos