Madiwani Temeke wataka miradi yenye ubora

DAR E SALAAM: BARAZA la Madiwani Manispaa ya Temeke limewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi wilayani humo kufanya hivyo kwa ubora na wakati.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke, Uzairu Athumani amesema hayo leo Mei 26, 2026 wakati wakipokea taarifa ya robo ya mwaka wa tatu katika wilaya hiyo 2025/26 na kusema kuwa halmashauri hiyo inawapa kipaumbele wakandarasi wazalendo ili kukuza uchumi wa ndani.
“Baraza limepokea na kujadili taarifa za shughuli za maendeleo kata zote zikihusisha sekta ya elimu ,afya barabara uzoaji a taka na miundombinu tumezijadili kwa umakini tumetoa maelekezo kwa wataalam wetu wazikamilishe kama walivyopendekeza watendaji na waheshimiwa madiwani,”
“Sisi aliyelipa kodi kwetu tunamuona ni mshamba tofuati na ilivyozoeleka kwamba anayekwepa kodi ndio mjanja kwa Temeke sasa anayelipa kodi ni mjanja wananchi wa Temeke sasa wanalipa kodi kweli kweli ndio maana tunatembea kifua mbele” amesema Uzairu.
Kwa Upande wake, Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Jomaary Satura amesema manispaa hiyo imeendelea kubuni vyanzo vipya vya mapato jambo litakalowezesha kujua kwa manispaa hiyo.


