Madiwani wahimizwa uwajibikaji dhidi ya rushwa

ARUSHA: KATIBU Tawala Wilaya ya Arusha Mjini, Jacob Rombo amewataka madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kusimamia suala la rushwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Rombo ametoa rai hiyo leo jijini Arusha mara baada ya zoezi la uapisho wa madiwani 34 wa Jiji hilo ambapo madiwani 25 walichaguliwa na madiwani nane ni wa viti maalumu.

Amesisitiza utawala bora ni muhimu katika kuwaletea maendeleo wnaanchi ikiwemo kuepuka suala zima la rushwa na kuagiza kuacha kuingilia kati majukumu ya watumishi wanaotekeleza ikiwemo suala la mipango miji

“Msiingiliane majukumu wakati wa utendaji kazi, Bali mfuate sheria na taratibu za halmashauri, simamieni viapo vyenu”

Wakati huo huo, diwani Muhsin Ramadan wa kata ya Sokon 1 na diwani wa viti maalum, Michelle Mrema walisema watasimamia vema majukumu yao ikiwemo kufanya kazi kwa ufanisi katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa kata 25 za Jiji la Arusha.

 

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I am making a good salary from home $7580-$9065/week , which is amazing, under a year ago I was jobless in a horrible economy. I thank God every day I was blessed with these instructions, Definitely a try..

    See This Link………………………………….. http://Www.Cash43.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button