Maelfu wamzika kiongozi wa Hamas

ISRAEL: Maelfu ya watu wamejitokeza kwenye mazishi ya kiongozi wa kisiasa wa Hamas, Ismail Haniyeh, nchini Iran ambaye aliuawa katika shambulizi mjini Tehran.

Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameongoza sala hiyo kabla ya kiongozi huyo kuzikwa nchini Qatar.

Vyombo vya habari vya Marekani vimewanukuu maafisa wa Iran wakisema kiongozi huyo mkuu aliamuru shambulio la moja kwa moja dhidi ya Israel, na ndio chanzo cha shambulio lililotokea nchini Iran.

Advertisement

Hata hivyo, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema nchi yake imelipiza kisasi kwa maadui zake wanaoiandama Israel.

“Tangu kutokea kwa shambulizi Beirut, tumesikia vitisho kutoka pande zote,” amesema.

SOMA: Kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh auawa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa tahadhari huenda mapigano katika ukanda wa Gaza yanaweza kuongezeka.