Mageuzi yaja taasisi teknolojia ya ujenzi

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema serikali imetenga fedha kiasi cha Sh bilioni 5.9 kwa ajili ya ujenzi wa jengo moja la taaluma lenye ghorofa nne katika makao makuu ya Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) – Morogoro.

Amesema  kuwa jengo hilo licha ya matumizi mengine ,litakuwa na ofisi za idara za kitalauma na madarasa yanayowezesha kutoshereza wanafunzi 1,001.

Naibu Waziri amesema hayo mbele ya  wajumbe wa Kamati  ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake, Selemani Kakoso kupitia taarifa yake wakati wa kukagua  maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo moja la taaluma lenye ghorofa nne eneo la makao makuu ya taasisi hiyo mkoani Morogoro.

Amesema  jengo hilo linasimamiwa na Mhandisi mshauri Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na Utekelezaji wake unafanywa na mkandarasi M/s B.H Ladwa Limited ,Morogoro na  mradi huo ulianza Juni Mosi ,2023 na uliopaswa ukamilike Mei 31, 2024.

Mhandisi Kasekenya amesema tayari mkandarasi amelipwa Sh bilioni 1.8 sawa na asilimia 31.7 ya fedha iliyolipwa  ingawa kwa sasa ameongezewa muda miezi nane hadi Septemba 30, 2025.

Naibu Waziri amegakikishia Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge kuwa, kuwa wizara imepokea ushauri ,maboresho na maelekezo katika kusimamia ujenzi huo ili kuweza kukamilika kwa wakati.

Kwa upanade wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo ,Selemani Kakoso amesema Kamati yake imelidhishwa na kasi ya ujenzi huo na kumpongeza mkadarasi kwa kazi yake nzuri chini ya wasimamizi TBA na kutaka maboresho mengine ambayo yameshauriwa na wabunge yakafanyiwe kazi.

Kakoso amesema kuwa endapo watasimamia vizuri ujenzi na fedha zimazotolewa na Rais wataijengea heshima nchi ,kuijengea heshima wizara kwani asilimia kubwa ya mradi huo umetokana na kusimamiwa na Bunge .

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button