Magori Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi Simba

MWEKEZAJI na Rais wa Simba ya Dar es Salaam, Mohamed Dewji amemteua Crescentius Magori kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo.

Taarifa kwa umma aliyoitoa Dewji usiku huu imeeleza kuwa kwa muda mrefu amekuwa akihudumu kama Rais wa Simba na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, lakini kutokana na majukumu yake mengine ya kikazi na wakati mwingine anakuwa yupo mbali, hivyo sasa jukumu la uenyekiti linahitaji mtu aliye karibu na mwenye muda wa kutosha.

Pia taarifa imesema ameteua Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba upande wa mwekezaji na kuwataja kuwa ni Rashid Shangazi, Barbara Gonzalez, Hussein Kitta, Azim Dewji, Rashid Shangazi, Swedi Mkwabi, Zully Chandoo na George Ruhanga.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button