Mahakama Itilima, Busega kuzinduliwa rasmi

MAHAKAMA za Wilaya ya Busega na Itilima mkoani Simiyu zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho ijumaa Novemba 24, ikiwa ni jitihada za Serikali kusogeza huduma za Kimahakama na kusikilizwa kwa mashauri kwa wakazi wa Wilaya hizo mbili.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Caroline Kiliwa akizungumza leo Novemba 23,2022 amesema wakazi wa halmashauri hizo waliokuwa wakilazimika kusafiri kilomita 120 kufuata huduma hizo katika halmashauri nyingin.

“Yale mashauri yote yaliyofunguliwa kabla ya kufunguliwa kwa Mahakama ya Busega yataendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Bariadi na yale mapya yatakayo funguliwa baada ya uinduzi huo yatasikilizwa katika halmashauri ya wilaya ya Busega na Itilima.” Amesema

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button