Mahendeka: Changamoto kubwa Tasaf ni wanasiasa

WAFANYAKAZI wa Mfuko wa  Maendeleo ya Jamii (TASAF) wametakiwa kufanya kazi kwa ueledi na kuzingatia maadili huku wakiepuka ubaguzi wa aina yoyote katika utekeleaji wa majukumu yao.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ikulu, Mululi Mahendeka  akifungua Mkutano wa Mwaka wa wafanyakazi hao uliofanyika  katika ukumbi wa APC Bunju, Dar es Salaam,

Mahendeka, amesema moja ya changamoto zinazoukabili mfuko huo ni baadhi ya wanasiasa kupotosha lengo halisi la Mfuko na kuhusisha kazi zake na itikadi za kisiasa na ukabila.

Amesema, kwa kuwa wako wanasiasa, kwa malengo wanayoyajua wao, wamekuwa wakieneza habari potofu kuwa kazi wa Mfuko zinahusiana na ikitadi za kisiasa, ni jukumu la wafanyakazi hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa kufuata taratibu zilizopo na hivyo kuepuka ubaguzi wa itikadi za kisiasa, kidini na kikabila.

“TASAF ni taasisi ya Serikali na hivyo inafuata taratibu za kiserikali.

buy clomid online https://psychotherapy.com/wordpress/img/jpg/clomid.html no prescription pharmacy

Hakikisheni mnafanya kazi kwa bidii ueledi na maarifa. Fuateni miongozo ya serikali ikiwemo kutunza siri za Serikali,” amesema.

buy advair online https://psychotherapy.com/wordpress/img/jpg/advair.html no prescription pharmacy

Aidha, ameitaka menejienti ya TASAF kutambua majukumu yake na kuyatekeleza kwa ukamilifu, kutembelea miradi katika mamlaka za utekelezaji, kuzungumza na walengwa na kujua changamoto zao ili iwe rahisi kuzitatua.

“Fanyeni kazi sawasawa na jina la mfuko na muweke kipaumbele kwa maendeleo ya jamii,” amesema.

Amewataka kwafanyakazi kutunza rasilimali za taasisi ikiwemo magari, kompyuta, mifumo na kompyuta mpakato na kufanya kazi zilizopo  kulingana na sera kukidhi matarajio ya Serikali kwa mfuko huo

“Mambo ya uendeshaji wa miradi yameainishwa vizuri katika andiko la mradi lililosainiwa kati ya Serikali na wadau wa maendeleo. Someni andiko la mradi kwa makini ili mjue mnachotarajiwa kufanya,” amesema.

buy reglan online https://psychotherapy.com/wordpress/img/jpg/reglan.html no prescription pharmacy

Akitoa shukurani kwa Katibu Mkuu, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Kitaifa ya TASAF, Peter Ilomo amesema Kamati yake na Menejimenti inazingatia maelekezo hayo na wakati wa mkutano kama huo watatoa mrejeshokuhusu utekelezaji wa maelekezo.

Habari Zifananazo

Back to top button