Majaliwa aagiza kikosi kazi TRA kiondolewe Kariakoo

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza kuondolewa kwa kikosi kazi cha ukusanyaji wa mapato katika eneo la Kariakoo akida kuwa uwepo wa kikosi hicho ni kinyume na maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan.
–
Majaliwa amesema hayo leo Mei 15, 2023 wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Kariakoo, ikiwa ni hatua ya pili ya kusuluhisha mgomo huo baada ya ile ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla kushindikana asubuhi.
–
“Tuna taarifa za kikosi kazi kimeundwa, kinazunguka humu ndani ( Kariakoo ) pamoja na kazi nzuri inayofanywa katika kukusanya kodi, lakini Rais Samia alikemea suala la kikosi kazi,” amesema Majaliwa.
–
Asubuhi ya leo wafanyabiashara hao waligoma kufungua maduka kwa madai ya utitiri wa kodi na tozo walizodai kutokuwa rafiki.
–
Taarifa ya awali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ilieleza kuwa Majaliwa alipanga kukutana na uongozi wa jumuiya hiyo Mei 17, 2023 katika ukumbi wa Anatouglou uliopo Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.