Majaliwa aitaka TANAPA kujipanga watalii kutoka Urusi

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Mamlaka ya hifadhi za Taifa (TANAPA) kuandaa mazingira rafiki kwa ajili ya watalii kutoka Urusi wanaotarajiwa kuanza kuingia nchini.

Majaliwa ameyasema hayo Agosti 03, 2023 wakati akitembelea mabanda mbalimbali katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ‘Nane Nane 2023’ yanayoendelea jijini Mbeya ikiwa leo ni siku ya tatu ya Maonesho hayo.

Waziri Mkuu amesema kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita wakati ndege za Urusi zikitua, Tanzania ilipokea idadi ya watalii zaidi ya elfu 72 kutoka Urusi kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Advertisement

Aidha ameongeza kinachosubiriwa kwa sasa ni taratibu za makubaliano baina ya nchi hizo mbili kabla ya watalii kutoka Urusi kuanza kuingia Tanzania.

11 comments

Comments are closed.