WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa leo Oktoba 26, 2024 amekabidhi magari mapya 10 ikiwa ni ishara ya kukabidhi magari 88 yaliyonunuliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili kuboresha utendaji kazi wa taasisi hiyo.
Akitoa taarifa ya magari hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Crispin Chalamila amemweleza Waziri Mkuu kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, taasisi hiyo imepatiwa jumla ya Sh bilioni 30 za kununulia magari 195 ambapo 88 yameshanunuliwa.
WAZIRI MKUU AIKABIDHI TAKUKURU MAGARI 88
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 26,2024 amekabidhi magari mapya 10 ikiwa ni ishara ya kukabidhi magari 88 yaliyonunuliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini-TAKUKURU
Bofya link kusoma zaidihttps://t.co/q4bQQFj2L1 pic.twitter.com/bAXlcwfDHd
— Ofisi ya Waziri Mkuu (@TZWaziriMkuu) October 26, 2024
“Mchakatio wa kununua magari 107 yaliyobakia unaendelea na tunatarajia kuyapata hivi karibuni, tunaahidi kutatunza magari haya ili kuongeza tija katika utendaji wetu,” amesema Crispin.
Waziri Mkuu amekabidhi magari hayo wakati anafunga mafunzo ya awali ya uchunguzi ya Takukuru, hafla iliyofanyka Shule ya Polisi Tanzania, Moshi mkoani Kilimanjaro.