Majaliwa akaribisha wawekezaji wa Italia

ITALIA; WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa nchini Italia kuja Tanzania kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa kuwa Tanzania ina malighafi za kutosha pamoja na uwepo wa masoko ya uhakika kutokana na eneo la kijiografia.

“Msisitizo wa Mheshimiwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan na mkakati wa serikali ni kuwahamasisha wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa mbalimbali nchini waje kuwekeza katika ujenzi na kuzalisha bidhaa hizo nchini ili zipatikane kwa wingi na kwa urahisi,” amesema Waziri Mkuu leo Alhamisi, Oktoba 19, 2023.

Alikuwa akizungumza katika Jukwaa la Tatu la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Italia lilifanyika Palazzo Regione Lombardia, Milan nchini Italia.

Waziri Mkuu yuko nchini Italia akimuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Chakula Duniani ulioanza Oktoba 16 hadi Oktoba 20, 2023, Rome nchini Italia.

Waziri Mkuu ametaja baadhi ya maeneo ambayo wawekezaji hao wanaweza kuja kuwekeza katika sekta za madini, kilimo, mawasiliano, mifugo, uvuvi, utalii na afya hivyo amewakaribisha wafanyabiashara hao na wawekezaji watumie fursa hiyo na kuwekeza nchini.

Amesema licha ya Tanzania kuwa na maeneo na mazingira mazuri ya uwekezaji pia amesema nchi ina vivutio vingi vya utalii hivyo, amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara na kampuni za mawakala wa utalii waje nchini na kuwekeza katika ujenzi wa hoteli za kitalii katika miji mbalimbali yakiwemo majiji ya Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma.

Amesema kwa sasa serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa, barabara, viwanja vya ndege na nishati ya uhakika ili kurahisisha shughuli mbalimbali zikiwemo za uwekezaji.

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Italia, Balozi Mahmoud Thabit Kombo ametumia fursa hiyo kuwahakikishia ushirikiano wawekezaji na wafanyabiashara wote kutoka nchini Italia ambao watahitaji kuwekeza na kufanya biashara nchini Tanzania.

Jukwaa hilo la Tatu la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Italia limehudhuriwa na wafanyabiashara na wawekezaji zaidi ya 300 kutoka mataifa hayo. Pia, mbali na wafanyabiashara na wawekezaji pia limehudhuriwa na Wakurugenzi na Wakuu wa Taasisi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Taasisi hizo ni pamoja Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Kukuza ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) ambao viongozi wake walipata fursa ya kutaja fursa za uwekezaji zilizopo nchini pamoja na namna ya kuwawezesha kuyafikia maeneo hayo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Julia
Julia
1 month ago

We started Work with Google all the way from the beginning. Everybody can come in together and work on these shared documents, Join Work As Well Today And Take Income
Just Go This Link Click It….> > > http://www.Smartcash1.com

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x