Majaliwa amwakilisha Rais Samia Tunisia

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa TICAD unaotarajiwa kufanyika Agosti 27 na 28 nchini Tunisia.

Mkutano huo ni muhimu katika kupanga mikakati ya Ushirikiano na ajenda za maendeleo kati ya Japan na Afrika.

Tanzania imekuwa ikinufaika na utekelezaji wa miradi mbalimbali katika sekta za miundombinu ya barabara, nishati ya umeme, maji, elimu, afya na kilimo.

Mkutano huu unafanyika Afrika kwa mara ya pili tangu mwaka 1993. Mara ya kwanza ulifanyika Nairobi, Kenya mwaka 2016.

Katika Mkutano wa saba uliofanyika Yokohama, Japan mwaka 2019, Japan ilitenga Dola za Marekani bilioni 20 kwa ajili ya kufanikisha malengo mbalimbali katika kipindi cha miaka mitatu (2019 -2022). 

Habari Zifananazo

Back to top button