Majaliwa ataka mshikamano kukuza michezo

Majaliwa ataka mshikamano kukuza michezo

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amezitaka Nchi za Umoja wa Afrika (AU) wa Baraza la Michezo Kanda ya Nne Afrika, kushikamana na kushirikiana kukuza michezo, lengo likiwa kuitangaza kanda hiyo kimataifa katika fani za michezo mbalimbali.

Majaliwa amesema hayo leo wakati akifungua Mkutano wa Mawaziri wa Michezo ,Utamaduni na Sanaa wa Nchi 14 za Afrika Kanda ya Nne unaofanyika jijini Arusha na kusema kuwa njia pekee ya kukuza michezo ni kwa nchi hizo kushikamana na kushirikiana, kwani hakuna mafanikio ya njia ya mkato.

Alisema Kanda ya Nne Afrika katika kukuza michezo Inawezekana na siri ya kukuza michezo ni kushirikiana kwa nchi zote za ukanda huo na nchi yoyote ikiwa inafanya vizuri katika mchezo fulani, basi inapaswa kuungwa mkono kwa dhati.

Advertisement

Amesema kila nchi awekeze kujenga uwekezaji wa michezo na kupiga vita kushika mkia katika mashindano, hivyo ni wajibu kuweka mikakati ya pamoja kukuza michezo katika ukanda huo.

” Tunahitaji kushikamana na kushirikiana katika fani ya michezo na mshikamano huo uweze kuigwa na kanda nyingine za Afrika na ikiwezekana tuweze kufanya vizuri katika michezo ngazi ya dunia,” alisema Majaliwa

Naye Waziri wa Utamaduni , Sanaa na Michezo,Dk  Pindi Chana kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu  alisema kuomba Tanzania kuwa Makao Makuu ya Sekretarieti ya Baraza la Umoja wa Afrika Ukanda Kanda ya Nne ni mwendelezo wa maono ya watangulizi wake yanayothibitisha utayari ambao serikali inao na kujipanga kutoa huduma stahiki kwa mafanikio ya sekta ya michezo.

Dk chana alisema kuwa mkutano huo wa siku moja wa mawaziri utakuwa na agenda maalum zinazolenga kutoa mwelekeo na mustakabali wa sekta ya michezo kwa nchi wanachama wa Kanda ya Nne na moja ya agenda mahsusi ni  pamoja na mkutano huo kupitisha mpango kazi wa baraza na mawaziri , kupitisha makao makuu ya sekretarieti ya baraza hilo.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *