Majaliwa atembelea kiwanda cha kuchakata mazao ya misitu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo, Machi 21 amewasili mkoani Njombe ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa Mgeni Rasmi katika kilele cha Siku ya Misitu Duniani inayofanyika kitaifa mkoni humo.
Baada ya kuwasili Waziri Mkuu ametembelea kiwanda cha uchakataji mazao ya misitu cha TANWAT (Tanganyika Wattle Company Limited) kilichopo Njombe mjini ambapo ameshuhudia shughuli mbalimbali zinazofanywa na kiwanda hicho.
Akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho Waziri Mkuu amewasihi wafanyakazi wa kiwanda hicho kufanya kazi kwa weledi ili kufanikisha malengo ya muwekezaji.
“Fanyeni kazi kwa uaminifu, fanyeni kazi kwa uadilifu, na kwa weledi,” amesema.
1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *