Majaliwa awataka viongozi CCM kusimamia miradi

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi-CCM mkoani Kigoma kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa viwango vinavyokubalika na kuleta tija kwa wananchi.

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM, Livingstone Lusinde amesema hayo kwa niaba ya Majaliwa ambaye ni Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa chama mkoa wa Kigoma wilayani Kakonko katika kilele cha maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa CCM ambayo kimkoa yanafanyika wilayani humo.

Majaliwa amebainisha kuwa serikali imetoa fedha nyinyi mkoani humo hivyo ni lazima fedha hizo zilete matokeo katika Maisha ya wananchi.

Waziri Mkuu amesema zaidi ya shilingi Trilioni 11.4 zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hivyo viongozi wa CCM wana jukumu la kuitembelea, kuikagua, kuisemea miradi hiyo.

Mkuu wa Wilaya Kakonko, Evance Mallasa

Awali Akitoa taarifa ya mkoa Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma, Christopher Pallangyo amesema hali ya chama mkoani humo imeimarika na imeshinda nafasi za serikali za mitaa kwa asilimia 96 na kwamba wana uhakika uchaguzi wa mwaka huu wa madiwani, wabunge na Rais watafanya vizuri.

Katibu wa CCM mkoa Kigoma Christopher Pallangyo

Pallangyo amesema Kigoma imepiga hatua kubwa kwenye maendeleo kutokana na kutekelezwa kwa miradi hiyo ikiwemo ya barabara ambapo kwa sasa mradi wa barabara ya kiwango cha Lami kutoka Kigoma hadi Nyakanazi kilometa 360 inakaribia kukamilika huku sehemu kubwa ya barabara hiyo ikipitika kwa lami.

Naye Mkuu wa wilaya Kakonko Evance Mallasa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye amesema serikali chini ya usimamizi wa CCM imefanya kazi kubwa katika utekelezaji wa miradi ya wananchi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button