Majaliwa mgeni rasmi kongamano la uhandisi

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la 32 la Kitaifa la Ubunifu wa Uhandisi litakalofanyika Novemba 30 mpaka Disemba 2, 2023 Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari, Rais wa Taasisi ya Wahandisi Tanzania, Dk Gemma Modu ameyahimiza makampuni kuungana ili kuingia katika soko la ushindani wa tenda mbalimbali.

Advertisement

Dk Modu amesema Dhima ya mkutano huo ni “Innovative solutions in Engineering for Sustainable Development” ambapo kwa tafsiri ni “Suluhisho za Ubunifu katika Uhandisi kwa Maendeleo Endelevu”

Dk Modu Ameongeza kuwa lengo ni kuweza kuendana na kukidhi matakwa ya maendeleo Teknolojia na kuweza kusiadia Nchi kutatua changamoto katika sekta mbalimbali za kiuchumi pia kutoa Suluhisho la matatizo katika jamii.

Naye Mjumbe wa Baraza la Utendaji wa IET mhandisi Pendo Haule amesema aliwaomba na kuwahimiza maoampuni ya wazawa kujitokeza kuchukua Miradi pindi inapotangazwa ilu kuonesha ujuzi na utaalamu wao.

2 comments

Comments are closed.