Majaliwa: sitaki wababaishaji, vishoka

DODOMA: WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wathamini wote wawe waadilifu, wenye weledi na wazingatie miiko ya taaluma katika kazi zao za kila siku.

Majaliwa ameyasema hayo Novemba 9, 2023 akifungua Mkutano Mkuu wa Nne wa Mwaka wa Wathamini uliofanyika mjini Dodoma.

Amesema, wathamini ni watu muhimu katika kufanikisha mipango ya maendeleo ya Taifa hivyo wanapaswa kuwa waadilifu na kuzingatia thamani halisi ya ardhi, jengo au chochote kinachofanyiwa uthamini.

“Kazi ya uthamini si ya wababaishaji au vishoka, hivyo basi kila mthamini hana budi kuthamini na kuheshimu taaluma yake,”amesema Majaliwa na kuongeza

“Wapo baadhi ya wathamini ambao si waadilifu kwa kushirikiana na watendaji wengine hutoa makadirio ambayo hayawiani na thamani halisi. Vitendo hivyo husababisha kupoteza mapato ya Serikali lakini pia kuwanyima haki wale wanaostahili kupata haki,”amesema.

Aidha, Majaliwa amewataka watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi hususani wathamini washirikiane na sekta binafsi kufanya kazi za uthamini.

“Tumieni fursa ya uwepo wa wathamini binafsi ili kutoa huduma bora na ya haraka hapa nchini, kufanya hivyo mtakuwa mnatekeleza maagizo ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan ya ushirikishaji wa sekta binafsi kwa maendeleo ya Taifa,”amesema.

Naye, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geoffrey Pinda amesema kuwa uthamini wa fidia ni ufunguo wa maendeleo na mabadiliko chanya ya kiuchumi kwa kuwa unawezesha wawekezaji kupata ardhi na kuwekeza mitaji yao.

Amesema kuwa Wizara kwa kushirikiana na Bodi ya Usajili wa Wathamini nchini imejipanga kuhakikisha shughuli zote za uthamini zinaboreshwa.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
7 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
NAMONGO FC
NAMONGO FC
23 days ago

IKIFIKA WALIOPO HAWATOSHI… WATANZANIA 3 WANATAFUTWA… 1. MKULIMA MKUBWA (TAASISI ZA SERIKALI) 2. MKULIMA WA KATI (MWEKEZAJI MKUBWA SANA) 3. MKULIMA MDOGO (ANAYELIMA NYUMBANI)..

336385342_23852687669090184_4327056666681808736_n-1699524871.7938-300x300.jpeg
NAMONGO FC
NAMONGO FC
23 days ago

IKIFIKA WALIOPO HAWATOSHI… WATANZANIA 3 WANATAFUTWA… 1. MKULIMA MKUBWA (TAASISI ZA SERIKALI) 2. MKULIMA WA KATI (MWEKEZAJI MKUBWA SANA) 3. MKULIMA MDOGO (ANAYELIMA NYUMBANI)..

400691249_864990868631687_149643332150728266_n-1699514610.2614-1699523863.3682-212x300.jpg
NAMONGO FC
NAMONGO FC
23 days ago

IKIFIKA WALIOPO HAWATOSHI… WATANZANIA 3 WANATAFUTWA… 1. MKULIMA MKUBWA (TAASISI ZA SERIKALI) 2. MKULIMA WA KATI (MWEKEZAJI MKUBWA SANA) 3. MKULIMA MDOGO (ANAYELIMA NYUMBANI)…

400652614_122123967464061853_6811123058608430011_n-1699514588.5978-200x300-1699523844.9688.jpg
NAMONGO FC
NAMONGO FC
23 days ago

IKIFIKA WALIOPO HAWATOSHI… WATANZANIA 3 WANATAFUTWA… 1. MKULIMA MKUBWA (TAASISI ZA SERIKALI) 2. MKULIMA WA KATI (MWEKEZAJI MKUBWA SANA) 3. MKULIMA MDOGO (ANAYELIMA NYUMBANI)…..

396913935_270519422649565_3279129179102033513_n-1699514567.7649-232x300-1699523827.9501.jpg
NAMONGO FC
NAMONGO FC
23 days ago

USALAMA KAZI MHE TUTAFANYA KWA AJILI YA “MLIMA KILIMAJARO” – LAZIMA TUFANYE KITU KWA AJILI YA TANZANIA USALAMA WETU TUKITEMBELE

OSK-1699526502.5327-300x200.jpeg
AlmaRankin
AlmaRankin
23 days ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website________ http://Www.Careers12.com

Last edited 23 days ago by AlmaRankin
Angila
Angila
22 days ago

I get paid over $87 per hour working from home with (Qz)2 kids at home. I never thought I’d be able to do it but my best friend earns over 10k a month doing this and she convinced me to try. The potential with this is endless. 
.
.
.
.
Here’s what I’ve been doing…> > > http://remarkableincome09.blogspot.com

Back to top button
7
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x