KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa(CCM-NEC), Itikadi Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amempongeza Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu kwa kuwa muwazi kusema kuwa hawawezi kusimamisha wagombe kila kijiji, mtaa na kila kitongoji.
Makalla ameyasema hayo leo Novemba 6,2024, huku akizungumzia namna CCM ilivyojipanga kushika dola kwa kusimamisha wagombea kila mtaa, kijiji na vitongoji nchi nzima.
“Jana Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu lisu amesema wao hawawezi kusimamisha wagombe akila sehemu na Tundu Lisu nampongeza kwa sababu amekuwa mkweli kuliko mwenyekiti wake,”amesema Makalla.
Ameongeza kuwa tafsiri yake ni kwanza Chadema hawpo tayari kushika dola maana dola haishikwi kwa kuweka wagombea wachachi, hivyo CCM imethibitusha ipo tayari kushika dola kwa kuweka wagombea kila sehemu.