Makalla ataka hamasa daftari la kudumu wapiga kura

DAR ES SALAAM: KATIBU wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amewataka mabalozi na kamati za siasa katika ngazi mbalimbali kufanya uhamasishaji kujiandiskisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Katika Mkoa wa Dar es salaam watu wanatarajiwa kuanza kujiandiskisha katika daftari la kuduma la mpiga kura kuanzia Machi 17 hadi Machi 23, mwaka huu.

Makalla ambaye pia Mlezi wa Mkoa wa Dar es Salaam ameeleza hayo leo Machi 5, 2025 alipozungumza katika mkutano wa viongozi wa chama na jumuiya ngazi ya shina, tawi, kata na wilaya katika Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku tano katika mkoa huo.

Makalla amesema utekelezaji siku zote huwa unaanzia katika ngazi ya chini na mabalozi ndo wanaishi na wananchi katika maeneo yao hivyo wanawajua vyema na ni rahisi kwao kuwafikia na kuwahamasisha.

“Mabalozi nyie ndo mnaishi na wananchi wetu huko mabalozi ndiyo walezi wa wanachama wa CCM, wanachama wapo katika mashina na matawi, mashina yakifanya kazi vizuri tawi, kata, wilaya, mkoa na sisi tukikaa huku taifa tunakuwa tunajua wanachama wetu wanalelewa vizuri na mabalozi,” amesema Makalla.

Ameongeza; “Nataka mabalozi wafanye kazi katika maeneo yao kazi nzuri ya uhamasishaji tuifanye matawi, kata jumuiya za chama, wakina mama vijana fanyeni uhamasishaji na sisi tunaamini utekezaji unafanyika zaidi katika ngazi ya chini, huko ndo walipo watu”.

Ameongeza kuwa lengo la chama cha siasa ni kushika dola na ili chama kiweze kushika dola kinatakiwa kushinda chaguzi zote yaani uchaguzi wa serikali za mtaa na uchaguzi mkuu na katika kushinda uchaguzi wowote unahitaji nguvu ya kura nyingi ambazo zinapigwa ili kupata ushindi.

Aidha, amewasisitiza kufanya hivyo ili waweze kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu na kuwataka wasifanye makosa katika hilo kwani mkoa huo unaongoza kuwa na idadi kubwa ya wapiga kura kuliko mikoa mingine nchini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button