Makalla: Mkandarasi wa awali alichelewesha barabara Buchosa – Sengerema

BUCHOSA: KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema kuchelewa kwa utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya kuunganisha Buchosha na Sengerema ni kosa la mkandarasi aliyekuwepo awali.

Makalla ameeleza hayo leo Mei 21,2025 wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Buchosa na Mji wa Bukokwa wilayani Sengerema mkoani Mwanza akiwa njiani kuelekea Usagara kwa ajili Mkutano wa hadhara ikiwa ni miendelezo wa ziara yake Kanda ya Ziwa.

Makalla ameeleza hayo akijibu kero hiyo ya barabara iliyotolewa na mmoja wa wakazi Bukokwa, Peter Nyangala aliuliza juu ya ujenzi wa barabara hiyo ya Bukokwa hadi Sengerema kwa kiwango cha lamikatika barabara hiyo yenye takribani kilometa 50.

Aidha, Makalla ameeleza kuwa akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Rais Samia Suluhu Hassan alitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo na mkandarasi alipatikana na kuweka kambi tayari kwa kuanza kazi lakini hawakuridhishwa na utendaji wake kwani ulikuwa wa kusua sua wakaamua kumuondoa.

“Nikiwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Rais Samia alitoa fedha za kuunganisha barabara hii ya kuunganisha Sengerema na Buchosa na mkandarasi akaweka kambi lakini hatukuridhishwa na utendeji kazi wa mkandarasi na utaratibu wa mumuondoa umeshakamilika na mkandarasi mpya amepatikana,” amesema Makalla.

Akiwahakikishia utekelezaji wake Makalla ameahidi kuwa balozi mzuri wa kufuatilia kuhakikisha wanapata barabara nzuri ya lami kwa sababu alihusika kuhakikisha wanapata barabara nzuri.

Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Erick Shigongo amesema katika jimbo hilo wamepokea zaidi ya kiasi cha Sh bilioni 76.3 kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maendeleo ikiwemo barabara, elimu, afya na ujenzi wa chuo cha ufundi ambacho kwa mara ya kwanza kimepelekwa Buchosa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button