Makamu wa Rais akamatwa kwa rushwa

Makamu wa Rais wa Malawi, Saulos Chilima yuko nje kwa dhamana baada ya kukamatwa na hutuma za kupokea rushwa ili kutoa kandarasi za serikali.

Taasisi ya kupambana na rushwa nchini humo limethibitisha.

Taasisi ya Kupambana na Rushwa nchini Malawi ( ACB) imeeleza Chilima alipokea malipo ya Dola $280,000 na vitu vingine kutoka kwa mfanyabiashara wa Uingereza Zuneth Sattar kama malipo ya kuipatia kandarasi Serikali ya Malawi.

Ofisi hiyo inasema Chilima alipokea pesa hizo kati ya Machi 2021 na Oktoba 2021 baada ya kutoa kandarasi za Jeshi la Ulinzi la Malawi na Huduma ya Polisi ya Malawi kwa kampuni mbili zilizounganishwa na mfanyabiashara huyo.

Aidha makamu huyo wa rais anakabiliwa na mashtaka sita ya rushwa ikiwemo matumizi mabaya ya ofisa ,kujinufaisha na mikataba ya serikali na kushindwa kutoa ripoti kamili kwa maofisa wa ofisi hiyo.

Mwezi Juni, Rais wa Malawi Lazarus Chakwera alisimamisha madaraka ya makamu huyo wa rais baada ya Taasisi ya Kupambana na Rushwa ya nchi hiyo kumshutumu Chilima kwa kukubali kulipwa kandarasi za serikali.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkuu katika Mji Mkuu Lilongwe ilimpa Chilima dhamana.

Miongoni mwa masharti ya kuachiliwa kwake ni kuripoti kwa Taasisi ya Kupambana na Rushwa kila baada ya miezi mitatu.

Mawaziri kadhaa na mawaziri wa zamani tayari wamekamatwa kuhusiana na kesi hiyo, ambapo maafisa wa umma 53 wameshtakiwa kwa kupokea pesa kutoka kwa Sattar kati ya Machi na Oktoba 2021.

Chilima alishirikiana na Chakwera kushinda marudio ya uchaguzi wa urais wa 2020. Aliungana na Chakwera katika kupinga uchaguzi wa udanganyifu mwaka wa 2019, ambao ulisababisha kura iliyoidhinishwa na mahakama mwaka uliofuata ambapo Chakwera alimshinda kiongozi wa zamani Peter Mutharika.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button