Makamu wa Rais ataka kuombea viongozi, Bara, Visiwani

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemedi Abdulla amewaomba watanzania kuwaombea viongozi wa serikali zote mbili ili kudumisha umoja, amani na mshikamano wa kuimarisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Abdulla pia amewataka viongozi, wazee na wengine wenye elimu ya muungano kuwaelimisha vijana kuhusu muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili waendele kuenzi.
Abdulla ametoa rai hiyo leo tarehe 25 Aprili, 2025 katika maadhimisho ya miaka 61 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo yamefanyika leo Mkoani Mtwara.
“Niwaombe watanzania wenzangu tuendelee kuwaunga mkono viongozi wa taifa letu, kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu waendelee kudumisha amani na umoja wetu,” amesema.
Katika hatua nyingine, Abdulla amesema tangu kuanzishwa kwa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, taifa limepata maendeleo makubwa pande zote mbili.
Amesema mafanikio yamepatikana kutoka na umahiri, uimara na umoja ikiwemo amani ambayo imeimarishwa na viongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ametaja mkoa wa Mtwara ambapo serikali imefanya maendeleo makubwa kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, na kilimo.
“Serikali ya Muungano imeleta maendeleo makubwa, mfano kwenye elimu hii serikali ya awamu wa sita tu imetoa shilling bilioni 83.65 za elimu katika mkoa wa Mtwara, pesa hizo zimejanga, madarasa na miundombinu mbinu mingine ya elimu,” amesema.
It’s going to be end of mine day, except before ending I am
reading this great piece of writing to increase
my know-how.
Google pay 500$ per hour my last pay check was $19840 working 10 hours a week online. My younger brother friend has been averaging 22k for months now and he works about 24 hours a week. I cant believe how easy it was once I tried it out.
Just Open This Website……… https://Www.earnapp1.com