Makonda: Ni unafiki kumtofautisha Rais Samia, JPM

DAR ES SALAAM: KATIBU wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda amesema ni unafiki kujaribu kumtofautisha Rais Samia Suluhu Hassan na mtangulizi wake, hayati Dk John Magufuli kwa kuwa wote wapo katika mlengo mmoja.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, alipomuwakilisha Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi katika mapokezi ya ndege mpya nchini, Makonda amesema kuna wanasiasa wasio na nia njema waliokuwa pamoja na Rais Magufuli, lakini sasa wanamkana.

“Kuna kasumba ya kutaka kuwatofautisha Rais Samia na Dk Magufuli, kila anachofanya Rais Samia, ndio kile alichokuwa akikifanya Rais Magufuli,” amesema Makonda na kuongeza kuwa wote dhamira yao ni kuwaletea Watanzania maendeleo.

Habari Zifananazo

Back to top button