Malimbikizo ya michango yalipwe kabla Sept 30

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka waajiri kutuza kumbukumbu za malipo ya michango ya waajiriwa pamoja na kulipa malimbikizo ya michango ya watumishi na tozo katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ifikapo tarehe 30 Septemba 2023.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo Juni 28 katika hotuba yake, Majaliwa amesema baadhi ya taasisi zimekuwa zikichelewesha malipo au kutolipia kabisa huduma wanazozipata kutoka taasisi nyingine za serikali ikiwemo 38 huduma za maji, umeme, simu, pango na ujenzi na hivyo kuathiri utendaji wa taasisi husika.

“Ninazielekeza taasisi zote za serikali kulipia huduma wanazopata kutoka taasisi nyingine ikiwemo Shirika la Umeme (TANESCO), Shirika la Mawasiliano (TTCL), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Wakala wa Majengo (TBA) na Mamlaka za Maji ifikapo tarehe 30 Septemba 2023 ili kuepusha kukwamisha uendeshaji wa taasisi hizo.”amesema Majaliwa.

Habari Zifananazo

Back to top button