Mama lishe kuboresha huduma kupitia mikopo

KIGOMA: Mama na Baba lishe wanaofanya wanaouza chakula kwenye hotelini na kwenye migahawa wamejipanga kutumia fursa ya mikopo na uwezeshaji kutoka serikalini na wadau wa maendeleo kupitia Umoja wa Mama Lishe Tanzania (UMALITA) ili kuhakikisha huduma zao zinakuwa za viwango na tija kubwa.

Katibu Mwenezi wa Taifa na Mhamasishaji wa UMALITA, Rehema Sule alisema hayo mkoani Kigoma wakati wa kuhamasisha mama lishe kujiunga na umoja huo sambamba na kusimamia chaguzi za umoja huo kwa ngazi za wilaya na mkoa.

Sule alisema kuwa baada ya kuungwa mkono na Rais Samia kwenye mkutano wao wameanzisha mkakati wa kuhakikisha mama lishe na baba lishe wanasajiliwa nchi nzima na kujiunga na UMALITA na  kupata vitambulisho ambavyo vitakuwa ishara ya kutambulika kwao popote wanapoingia.

Mwenyekiti wa UMALITA Mkoa Kigoma, Revina Kachira alisema kuwa kwa sasa mama lishe na baba lishe Mkoa Kigoma wanafanya kazi kila mtu kivyake wakiwa na ushindani lakini kuwepo kwa umoja huo kutawezesha kuwaweka pamoja kuzungumzia changamoto zao na namna ya kupata fursa za mikopo, uwezeshaji lakini pia kazi kutoka serikalini na taaasisi mbalimbali katika kuhudumia chakula kwenye misafara na mikutano.

Akizungumza wakati kiongozi huyo wa UMALITA taifa alipofikia ofisini kwake kujitambulisha Ofisa Maendeleo ya Jamii katika Sekretariet ya Mkoa Kigoma anayeshughulikia makundi maalumu, Minza Edward alisema kuwa kuwepo kwa makundi maalumu ambayo yameungana na kuwa na utambulisho rasmi yanawapa nafasi nzuri ya kuwafikia kwa haraka zinapotokea fursa mbalimbali ikiwemo mafunzo ,uwezeshaji, mikopo na hata baadhi ya makundi yanapohitajika kwa shughuli maalumu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button