Mambo muhimu Yanga, USM Algers
KUELELEA mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika Yanga dhidi ya USM Algers hizi ni namba muhimu kuelekea mchezo huo mkubwa Afrika.
Kuanzia hatua ya makundi timu hizo zimecheza michezo kumi hadi sasa.
Yanga wameshinda michezo saba wamepoteza mchezo mmoja, na kutoa sare michezo miwili, huku USM Algers wakishinda michezo mitano, sare michezo mitatu na kupoteza michezo miwili.
Yanga wamefunga jumla ya magoli 15 hadi sasa kwenye michuano hiyo, mabao tisa wamefunga katika uwanja wa nyumbani, huku mabao sita wakifunga viwanja vya ugenini.
Yanga wameruhusu jumla ya mabao matano, mabao manne wameruhusu katika viwanja vya ugenini, huku wakiruhusu kufungwa bao moja kwenye uwanja wa nyumbani.
USM Algers wamefunga jumla ya mabao 17, mabao 13 wamefunga katika uwanja wa nyumbani huku mabao manne wakifunga kwenye viwanja vya ugenini.
USM Algers wameruhusu nyavu zao kuguswa mara nane, mabao saba wamefungwa katika viwanja vya ugenini huku wakiruhusu bao moja tuu kwenye uwanja wa nyumbani.
Jumapili ni fainali ya kwanza ya kombe la shirikisho Afrika baina ya timu hizo mbili zenye namba za kusisimua kwenye michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya klabu Afrika ,ambapo mchezo huo utapigwa Uwanja wa Benjamini Mkapa DSM na kisha mchezo wa mkondo wa pili kupigwa nchini Algeria Juni 3, mwaka huu.