Mambo shwari upigaji kura Zanzibar

ZANZIBAR : MKURUGENZI wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Thabit Idarous Faina, amesema upigaji kura ya mapema unaendelea vizuri visiwani Zanzibar.
Akizungumza na Daily News Digital kupitia mahojiano maalumu kwa njia ya simu, Faina amesema hali ya upigaji kura huo imekuwa na mwitikio mzuri kwa wahusika hao maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba.
“Siku ya leo zoezi limekwenda vizuri; vituo vya kupigia kura vimefunguliwa kwa wakati, na upigaji kura umeendelea kwa utulivu. Wananchi waliopangwa kupiga kura kwa mujibu wa sheria wamejitokeza na kutekeleza haki yao ya kupiga kura,” alisema. SOMA: Wanaopiga kura Zanzibar leo watajwa
Kuhusu maandalizi ya upigaji kura kesho amesema yamekamilika, ikiwemo vifaa vya uchaguzi na wasimamizi, ambao wamejipanga kuhakikisha jambo hilo linafanyika kwa ufanisi .



