Mambo yaiva Karibu Kili Fair 2024
ARUSHA; WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Angelah Kairuki, anatarajiwa kufungua maonesho ya Karibu Kili Fair 2024 yatakayofanyika Juni 7-9 Viwanja vya Magereza jijini Arusha.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kilifair Ltd, Dominic Shoo, wanunuzi wa kimataifa kutoka nchi zaidi ya 40 wanatarajiwa kuhudhuria.
Amesema ana matumaini makubwa maonesho ya mwaka huu yatakuwa mazuri kuliko ya mwaka uliopita kutokana na ongezeko la washiriki, lakini pia ubora wa vitu vitakavyokuwa kwenye maonesho