MWANZA; Meli ya Mv Mwanza Hapa Kazi Tu, imeanza majaribio ya awali katika Ziwa Victoria leo Machi 25, 2024, tukio linalohusisha wataalam wa ndani na wengine takribani 20 kutoka pande mbalimbali za dunia.
Baadhi ya wataalamu hao wanatoka nchi za Ujerumani, Ureno, Uholanzi, Ufilipino, Denmark na Korea Kusini.
Siku chache zilizopita wakati wa ziara za kamati mbalimbali za kudumu za bunge katika bandari ya Mwanza Kusini inapojengewa meli hiyo, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za meli (MSCL), Eric Hamiss, alisema: “Jaribio la awali litafanyika kwa siku mbili, Machi 25 na 26 na litahusisha wataalam tu, kwa sababu za kiusalama.”