Mshindi mashindano ya gofu CDF kupewa gari

DAR ES SALAAM; ZAIDI ya wachezaji 100 wa gofu wanatarajia kushiriki michuano ya Gofu ya Mkuu wa Majeshi ‘ NMB CDF Trophy 2024’.

Michuano hiyo ni sehemu ya kusherehea miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na pia kumuenzi Mkuu wa Majeshi (CDF), Jenerali Jacob Mkunda na yanatarajia kufanyika kuanzia Oktoba 4-6, mwaka huu viwanja vya gofu Ligalo, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,  Brigedia Jenerali mstaafu, Michael Luwongo amesema kuwa mashindano hayo yanatarajia kufanyika kwa kiwango kikubwa na pia zawadi ni za kiwango cha juu.

Advertisement

“Mshindi wa kwanza atapata zawadi ya gari aina ya Toyota Harrier yenye thamani ya Sh Milioni 75 na kiasi cha fedha taslimu Sh milioni 4 kutoka kwa wadhamini NMB.

Isome pia: Mambo yanoga mashindano gofu Lugalo

“Mashindano haya hufanyika kila mwaka lakini kwa mwaka huu yalipelekwa mbele na yatafanyika Oktoba kwa kuwa tulipisha sherehe za miaka 60 ya jeshi, lakini pia ikiwa ni sehemu ya kumuenzi Mkuu wa Majeshi,” amesema.

Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo cha wateja Maalumu NMB, Magreth Mallya amesema kuwa wametoa kiasi cha Sh Milioni 35 kudhamini michuano hiyo, huku Toyota wakitoa zawadi ya gari kwa mshindi,” amesema.

Naye Meneja Mkuu wa Toyota, Kadivi Williams amesema kuwa lengo la kutoa gari ni kutoa chachu ya wachezaji kupenda kucheza mchezo huo.

 

/* */