MAMCU yaingiza bil 207/- mauzo ya korosho

WAKULIMA wa Korosho kupitia Chama Cha Ushirika Cha Mtwara, Masasi na Nanyumbu (MAMCU) Mkoani Mtwara wameingiza shilingi bilioni 207 katika mauzo ya korosho ghafi tani 82 katika minada ya korosho inayoendelea nchini msimu 2025/2026.

Korosho hizo zimeuzwa kupitia Mfumo wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) katika minada mitatu iliyofanyika kuanzia Novemba 11 katika Wilaya za Nanyumbu, Masasi na Mtwara.

SOMA: Wakulima wa korosho watakiwa kuongeza mazao

Afisa Masoko wa MAMCU, Neema Sumavere amesema hayo katika mnada wa nne wa korosho uliyofanyika katika Halmashauri ya Mtwara.

Sumavere amesema korosho hizo ziliuzwa kwa sh 2700 bei ya juu na ya chini 2310 kwa kilo. Msimu 2024/2025 bei ya korosho kwa kilo ilikuwa sh 4120, bei ya chini ikiwa ni sh 3000

Alizungumza mara baada ya mnada wa nne kufanyika, Mjumbe wa MAMCU Seleman Mshamu amesema bei ya korosho msimu 2025/26 imekuwa chini kutokana na hali ya ubora wa korosho.

Amesema wakulima wengi wanapeleka korosho maghalani zikiwa na unyevunyevu jambo ambalo linashusha ubora wa korosho sokoni na kufanya wafanyabiashara wapange bei kulingana na ubora wa korosho.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button