Mkoa wa Lindi; mafanikio lukuki sekta ya kilimo
DESEMBA 11, mwaka huu katika Manispaa ya Lindi, kulifanyika Kongamano la Wataalamu wa Kilimo na Ushirika.
Kongamano hilo liliwashirikisha maofisa ugani, ushirika, maofisa kilimo ngazi ya mkoa, wilaya pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali ikiwemo vyama vikuu vya ushirika vya Runali na Lindi Mwambao. Wengine walioshiriki kongamano hilo ni wakurugenzi wa halmashauri za wilaya za Nachingwea, Ruangwa, Liwale na Halmshauri ya Manispaa ya Lindi.
Katika Kongamano hilo, Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Lindi, Harouni Kihara anawasilisha mapendekezo kadhaa kusaidia kuwezesha maofisa kufika kwa wakati katika mashamba ya wakulima wanapohitajika. Miongoni mwa mapendekezo hayo, ni pamoja na umuhimu kuwezesha maofisa ugani na kilimo kwa kuwapa uhakika wa mafuta na matengenezo ya vyombo vya usafiri.
Kihara anasema mambo hayo yatasaidia kuchochea uboreshaji wa shughuli na maisha ya wakulima mkoani Lindi na pia, kukuza uchumi wa mkoa na pata la taifa kwa ujumla.

Anasema: “Hali hiyo itasaidia kuwaondolea maofisa ugani au kilimo ulazima wa kutumia fedha za mishahara yao kununua mafuta au kugharimia matengenezo ya chombo cha kufanyia kazi alichokabidhiwa na mamlaka kuhudumia wakulima kwenye mashambani yao.”
Kwamba, wakati mwingine ofisa hulazimika kusafiri umbali mrefu kutoka kijiji kimoja hadi kingine ama kimoja, viwili au vitatu au zaidi ili kufika shambani kwa mkulima mwenye changamoto zinazohitaji utaalamu. Anasema kuwapo mazingira bora ya kazi yanayohusisha pia matengenezo ya gari au pikipiki, upatikanaji wa mafuta na ununuzi wa vitendea kazi ni mambo muhimu ili kukuza ufanisi wa kazi.
SOMA: Serikali yajizatiti utafiti, umwagiliaji kuinua kilimo
Anasisitiza umuhimu wa mkakati wa kuongeza uchumi, kuboresha maisha ya wakulima akisema hadi sasa kuna mazao matatu ya biashara yaani korosho, ufuta na mbaazi pekee na kwamba hayo pekee, hayatoi wigo mpana kwa mkulima kukua kiuchumi.
Anaongeza muktadha huo ipo haja ya kutambulisha na kuendeleza mazao mengine hususan choroko na dengu. Kwa mujibu wa Kihara, mpango huo unakusudiwa pia kutoa msukumo katika mazao ya matunda, mbogamboga na ufugaji ili kuongeza kipato. Anasema malengo mengine ya mkakati huo ni pamoja na kuimarisha uwajibikaji wa wataalamu wa sekta ya kilimo.
Unalenga pia kuwezesha kuwapo vikao vinne kila mwaka vya wataalamu pamoja na viogozi wanaosimamia kilimo katika halmashauri na kuwawezesha kushiriki vikao vya mipango na tathmini kuhusu maendeleo ya mazao ya korosho, ufuta na mbaazi.
Mengine ni kuongeza uzalishaji wa mazao ya korosho, mbaazi na ufuta kupitia ufuatiliaji, upatikanaji na usambazaji wa pembejo zikiwemo mbegu na miche sambamba na kusimamia mauzo ya mazao. Ofisa kilimo huyo wa Mkoa wa Lindi anasema katika kipindi cha miaka mitano ya 2020/2025, sekta ya kilimo mkoani hapo imepata mafanikio mengi.
Miongoni mwa mafanikio hayo anasema ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa korosho kutoka tani 65,812,94 mwaka 2020 hadi tani 115,680,505 zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 364.38 kwa mwaka 2025. Uzalishaji wa ufuta pia umeongezeka kutoka zaidi ya tani milioni 49.88 mwaka 2020 hadi zaidi ya tani milioni 75.76 zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 95.81 kwa mwaka 2025.
Kihara anasema pia kumekuwa na ongezeko la uzalishaji wa zao la mbaazi kutoka tani 5,038,093 mwaka 2020 hadi tani 35,449,249 zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 62.58 katika mwaka 2024. Kuhusu mazao ya chakula, ofisa huyo anabaianisha pia kuwa, kulikuwa na ongezeka la uzalishaji kutoka tani 462,409 mwaka 2020 hadi kufikia tani 491,214.5 mwaka 2025.

“Kwa upande wa mazao ya biashara, kulikuwa na ongezeko la kutoka tani 147,751,10 mwaka 2020 hadi tani 279,347.25 mwaka 2025,” anasema. Mafanikio mengine katika sekta ya kilimo katika kipindi hicho anasema ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya skimu za umwagiliaji kutoka 16 mwaka 2020 hadi skimu 18 mwaka 2025 sambamba na kuongezeka kwa eneo la umwagiliaji kutoka ekari 6,864 mwaka 2020 hadi ekari 8,301 mwaka 2025.
Katika kipindi hicho, mafanikio katika sekta ya kilimo mkoani Lindi hayaishi hapo tu, bali yanakwenda hadi katika uimarishaji wa huduma za ugani kwa kupata vitendea kazi.
Taarifa zinasema viendea kazi hivyo ni pamoja na magari mawili yaliyotolewa na Wizara ya Kilimo kwa ajili ya mkoa na Halmashauri ya Ruangwa na pikipiki 291 zilizotolewa kwa maofisa ugani wa halmashauri na mkoa, waratibu wa zao la korosho na maofisa ugani wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika pamoja na vipima udongo vinne.
Akiwasilisha taarifa katika kongamano hilo la wataalamu wa kilimo na ushirika, Mwakilishi wa Tume ya Taifa Umwagiliaji katika Mkoa wa Lindi, Shamili Karama anasema mkoa huo una eneo lenye ukubwa wa hekta 43,696.79 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji.
Eneo linalomwagiliwa kwa mazao ya mpunga na mbogamboga kwa sasa ni hekta 2,671.50 sawa na asilimia 6. Anasema skimu zinazofanya kazi ni 9 kati ya 16 zilizosajiliwa na tume kwa mujibu wa sheria. Anaongeza kuwa, vyanzo vikuu vya maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji ni mito inayotiririsha maji mwaka mzima.
Anasema Mkoa wa Lindi una miradi saba yenye thamani ya Sh bilioni 108.39 inayotekelezwa katika halmashauri sita ambayo kukamilika kwake kutanufaisha wakulima 2,194 kutoka vijiji 36 kwa kuongeza ekari 20,720 za kilimo cha umwagiliaji.
Anasema kati ya miradi hiyo, minne ni ya ujenzi wa mabwabwa na skimu za Nanganga (Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa), Narunyu, (Halamshauri ya Wilaya ya Mtama) pamoja na Rutamba na Mkwawa katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi. Mradi mwingine mmoja ni upembuzi yakinifu wa mabwabwa matatu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.




6.6 PROGRAMU ZA KIELELEZO
Mpango Elekezi 2050 umeainisha miradi 14 ya kielelezo. Miradi hii inalenga kuleta mageuzi ya viwanda nchini. Pia, itachochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali na uchumi wa kijani. Itasaidia kukuza nguvukazi yenye ujuzi na maarifa ya kisasa. Aidha, miradi hii inalenga kuongeza ushindani wa Tanzania katika masoko ya kikanda na kimataifa. Miradi hiyo imepangwa kama ifuatavyo:
NO PROGRAMME
1 Mageuzi ya Viwanda kwa Ukuaji wa Uchumi
2 Ujumuishaji wa Sekta ya Madini kwa Maendeleo ya Viwanda na Uchumi wa Kijani
3 Ubunifu wa Kidijitali na Miundombinu Mahiri kwa Ukuaji wa Siku za Usoni
4 Ujenzi wa Uhimilivu wa Tabianchi na Uchumi Endelevu wa Kijani
5 Kuendeleza Miundombinu na Muunganisho wa Usafiri kwa Tanzania kuwa Kitovu cha Kikanda
6 Mageuzi ya Sekta ya Nishati kwa Umeme Safi na Endelevu
7 Kukuza nguvukazi yenye Afya, Elimu na Ujuzi
8 Kuimarisha Utawala Bora, Uwajibikaji na Mifumo ya Udhibiti
9 Kuendeleza Miji Mahiri na Miundombinu Endelevu ya Mijini
10 Kuchochea Biashara, Uwekezaji na Upanuzi wa Uchumi
11 Kupanua Sekta ya Utalii na Uchumi wa Utamaduni
12 Kubadilisha Sekta ya Kilimo na Uchumi wa Vijijini
13 Kuboresha Elimu, Utafiti na Ubunifu wa Kiteknolojia
14 Mageuzi ya Kifedha ya Kidijitali na Jumuishi
6.6 PROGRAMU ZA KIELELEZO
Mpango Elekezi 2050 umeainisha miradi 14 ya kielelezo. Miradi hii inalenga kuleta mageuzi ya viwanda nchini. Pia, itachochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali na uchumi wa kijani. Itasaidia kukuza nguvukazi yenye ujuzi na maarifa ya kisasa. Aidha, miradi hii inalenga kuongeza ushindani wa Tanzania katika masoko ya kikanda na kimataifa. Miradi hiyo imepangwa kama ifuatavyo:
NO PROGRAMME
1 Mageuzi ya Viwanda kwa Ukuaji wa Uchumi
2 Ujumuishaji wa Sekta ya Madini kwa Maendeleo ya Viwanda na Uchumi wa Kijani
3 Ubunifu wa Kidijitali na Miundombinu Mahiri kwa Ukuaji wa Siku za Usoni
4 Ujenzi wa Uhimilivu wa Tabianchi na Uchumi Endelevu wa Kijani
5 Kuendeleza Miundombinu na Muunganisho wa Usafiri kwa Tanzania kuwa Kitovu cha Kikanda
6 Mageuzi ya Sekta ya Nishati kwa Umeme Safi na Endelevu
7 Kukuza nguvukazi yenye Afya, Elimu na Ujuzi
8 Kuimarisha Utawala Bora, Uwajibikaji na Mifumo ya Udhibiti
9 Kuendeleza Miji Mahiri na Miundombinu Endelevu ya Mijini
10 Kuchochea Biashara, Uwekezaji na Upanuzi wa Uchumi
11 Kupanua Sekta ya Utalii na Uchumi wa Utamaduni
12 Kubadilisha Sekta ya Kilimo na Uchumi wa Vijijini
13 Kuboresha Elimu, Utafiti na Ubunifu wa Kiteknolojia
14 Mageuzi ya Kifedha ya Kidijitali na Jumuishi