Man United, PSG kuvutana kumsajili Khvitcha Kvaratskhelia
TETEZI za usajili zinasema Manchester United inatarajiwa kushindana na Paris Saint-Germain katika kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Napoli na Georgia, Khvitcha Kvaratskhelia, mwenye umri wa miaka 23. (L’Equipe – in French)
Liverpool pia inaweza kumwania Kvaratskhelia iwapo Napoli itaamua kumruhusu kuondoka mwezi huu. (Athletic)
Wamiliki wapya wa Everton wanatarajiwa kumpa raia wa Scotland, David Moyes mwenye umri wa miaka 61 nafasi ya kurejea kuwa kocha Goodison Park. (Guardian)
West Ham United imeomba kufahamishwa kuhusu upatikanaji wa mshambuliaji Marcus Rashford na ina nia kumsajili kwa mkopo mchezaji huyo mwenye umri 27 kutoka Manchester United. (Talksport)
Pia klabu za Ligi Kuu ya Italia ya Serie A, AC Milan na Como zimeonesha nia kumsajili Rashford kwa ajili ya kipindi kilichobaki cha msimu huu. (Gianluca Di Marzio)
Arsenal haiwezi kumudu ada ya kuvunja rekodi ya uhamisho England inayohitajika kumsajili mshambuliaji wa Sweden, Alexander Isak, mwenye umri wa miaka 25 kutoka Newcastle United majira haya, huku beki wa kushoto wa Ukraine, Oleksandr Zinchenko, mwenye umri wa miaka 28, akiwa na uwezekano wa kuondoka Emirates mwezi huu. (Mail)



