Mangungu: Mo ni jasiri

Mangungu

DAR ES SALAAM: Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amesema Mohamed Dewji ‘Mo’ si mwekezaji tu katika klabu hiyo, bali ni mtu jasiri mwenye mapenzi nayo akiweka fedha.

Mangungu aliyasema hayo wakati akifanya mahojiano na kipindi cha michezo cha kituo cha redio cha Clouds FM cha mkoani Dar es Salaam.

“Simchukulii Mo kama mwekezaji tu, bali kama mtu jasiri aliyekubali kutumia fedha zake kuisaidia Simba,” alieleza Mangungu.

Advertisement

Alisema Simba inapitia changamoto kadhaa zilizosababisha baadhi ya viongozi kuamua kujiuzulu baada ya kujitathmini, na kuona kuwa wanapaswa kukaa pembeni.

SOMA: Miss Tanzania 2023 bado yupo yupo kwanza!

Viongozi waliojiuzulu ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya klabu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’ wajumbe wa bodi Rashid Shangazi na Zulfikir Chandoo wote kutoka upande wa mwekezaji.

Mangungu alisema baada ya ‘Try Again’ kutangaza kujiuzulu, alifanya mazungumzo na Mo aliyeridhia kurejea kwenye nafasi yake ya Uenyekiti wa Bodi.

Alisema amefahamiana na Mo kwa zaidi ya miaka 30, hivyo hana shida yoyote naye, na wamekuwa wakiwasiliana mara kwa mara kwenye mambo yote yanayoihusu Simba.