Manzese kuwa Kariakoo mpya

ENEO la Manzese lililopo Ubungo mkoani Dar es Salaam, linapaswa liwe la kimkakati biashara kama Kariakoo, kwa lengo la kuipatia Halmashauri ya Ubungo mapato mengi.

Akizungumza katika Kikao cha kuwasilisha rasimu ya Mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na mpango wa muda wa kati 2024/ 25 hadi 2026/27, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba ameeleza hayo.

“Ukitazama Manzese hapa inatuambia ni eneo la biashara kama ilivyo Kariakoo.

Advertisement

Tukiumiza vichwa vizuri eneo hili tutapata fedha.

“Pale fedha ni nyingi kama litatumika vizuri.

Tujenge mradi wa kimkakati uendane na jumuiko lililopo Manzese,” amesema.

Kuhusu hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Elias Ntiruhungwa amesema, ” Nimejitahidi kuchukua ushauri wote. Tumeupokea kama ulivyo tutaufanyia kazi kadri fedha zitakavyoruhusu,”.