Maofisa 7 wa Polisi kizimbani kwa mauaji

wasomewa maelezo ya awali

MAOFISA saba wa Jeshi la Polisi leo Agosti 9, 2023 wamesomewa maelezo ya awali, katika  kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini Mussa Hamis (25) inayowakabili.

Kesi hiyo namba 15 ya mwaka 2023 iliyopo  Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara inaongozwa na Jaji Mfawidhi Rose Ebrahim.

Awali, kesi hiyo, ilianza kutajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara Mei 4, mwaka huu  lakini baadae ilihamishiwa Mahakama Kuu ya Kanda ya Mtwara kutokana na mahakama hiyo ya mwanzo kutokuwa na hadhi ya kusikiliza.

Kesi hiyo inasikilizwa na jopo la mawakili wanne kutoka upande wa serikali na  10 kwa upande wa washtakiwa.

Wanaoshitakiwa ni Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Mtwara, Gilbert Kalanje, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, aliyekuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara, Charles Onyango, Mrakibu wa Polisi, aliyekuwa Mkuu wa intelijensia Mkoa, Nicholaus Kisinza, Mkaguzi wa Polisi, John Msuya, Mkaguzi msaidizi wa Polisi, Marco Mbuta, Mkaguzi wa polisi, Shirazi Ally Mkupa na askari na G5158 Kopro Salum Juma Mbalu.

Mashahidi 72, vielelezo vya maandishi visivyopungua 31 na vinavyoonekana vitano vinatarajia kuwasilishwa Mahakamani hapo.

Washtakiwa hao wote kwa pamoja wanashitakiwa kwa kumuua mfanyabiashara wa madini na Mkazi wa Kijiji cha Ruponda, wilayani Nachingwea Mkoa wa Lindi, Musa Hamis Hamis (25) siku ya Januari 5, 2022.

Habari Zifananazo

Back to top button