Maofisa halmashauri wafundwa

MTWARA: MAOFISA Biashara wa Halmashauri za mkoa wa Lindi na Mtwara wametakiwa kufanya shughuli zao kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati ya Maji Nchini (EWURA).
Akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo maofisa hao kuhusu kufahamu, shughuli zinazofanywa na Ewura, Meneja wa Kanda ya Mashariki Nyirabu Musira amesema kutokana na wao kuwa na majukumu mengi hususani ya kanda hiyo inasababisha kutokuwepo kila sehemu kwa wakati.
Amesema ni imani yake kuwa mafunzo yatakuwa yenye tija kwao huku lengo la mafunzo likiwa ni pamaoja na kuwawezesha maofisa hao kufanya shughuli zao kwa kusaidiana na Ewura, yaliyofanyika mkoani Mtwara.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Dk. Stephen Mwakajumilo amewataka pande hizo zote mbili kujadiliana kwa pamoja namna ya kutatua changamoto zinazojitokeza kwenye sekta ndogo ya mafuta.