Maonesho ya 77 yaja kidigitali

Bonyeza kitufe, uonyeshwe njia

MWAKANI wananchi watakaoudhuria maonesho ya sabasaba hawataangaika tena kusaka mabanda ya Taasisi au maduka yaliyomo kwenye maonesho hayo kwani kutafungwa mfumo maalum ambao utamuonyesha njia ya eneo analotaka kwenda.

Mfumo huo, utafungwa katika milango ya kuingilia ambapo mtu ataandika duka, banda au taasisi anayotaka kwenda na mfumo huo utaonyesha ilipo ili kuwapunguzia wananchi kutumia muda mwingi kuzunguka kutafuta banda  la mahali fulani.

Akizungumza leo Julai 8,2023 katika Kongamano la TEHAMA lililoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade), Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kwa sasa nchi ipo kwenye mchakato wa mwisho wa kuingia kwenye uchumi wa kidigitali na kuitaka Tantrade na Wizara anayoiongoza kufanya tathmini ya maonesho ya sabasaba ya mwaka huu mara yatakapomalizika Julai 13, 2023.

Amesema, tathmini itakayofanywa itoe  majibu ya namna ya kuboresha maonesho ya sabasaba ili mwakani yafanyike kwa mtindo wa kidigitali zaidi.

“Wananchi watakaotembelea hapa, wakute anuani za makazi, miundombinu iboreshwe , tumezoea kutembelea maeneo ya wenzetu, unaenda kweye kioo, unatype (kuandika)  duka au banda unalotaka kwenda unaonyeshwa njia, tunataka hivyo, na mimi naamini tunaweza.”Amesema Nape na kuongeza

“Tunataka watu wa digitali tuyateke maonesho haya, naamini inawezekana na nitasimamia, na ninataka nione mapendekezo namna maonesho yajayo yatakavyokuwa bora zaidi.”Amesisitiza

Amesema, Wizara imepewa  jukumu la kujenga uchumi wa kidigitali, hivyo  lazima kuwe na miundombinu bora ya taasisi ambayo itasimamia  kujenga uchumi wa  kidigitali.

“Ndio  maana tukaletewa TCRA, tumehimarisha tume ya Tehama, TTCL na yote tuliyofanya kwa TTCL ikiwemo kuwapa mkongo, kuwapa data center na Mungu akipenda Satelite tutapeleka  huko huko.

“Lakini posta, na mambo yote wanayofanya  ikiwemo  posta kiganjani na mengine, mageuzi tunayofanya  TSN, TCRA CCC ahadi yako kufanya mapinduzi na tunayasubiri, lakini pia tume ya taarifa binafsi, TBC na wengine wote hizi taasisi kwa pamoja tunashikamana kujenga uchumi wa kidigitali.”Amesema Nape.

Habari Zifananazo

6 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button