DAR ES SALAAM; LEO imetimia miaka minne tangu kifo cha Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kilichotokea katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam.
Ni kumbukumbu ya machozi kwa Watanzania kwa kumpoteza rais aliyekuwa madarakani na aliyefanya mambo mengi makubwa, yenye maendeleo kwa ajili ya taifa.
Anakumbukwa kwa msimamo wake wa kupambana na ufisadi, kuboresha miundombinu na kuhimiza uzalishaji wa ndani.
Aliendeleza vyema kazi za watangulizi wake katika sekta mbalimbali na kujielekeza kuhakikisha kwamba rasilimali za nchi zinanufaisha Watanzania wote.
Magufuli anakumbukwa alivyotekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kama vile ujenzi wa barabara na madaraja, pamoja na uimarishaji wa huduma za afya na elimu. Hakika Tanzania itaendelea kumkumbuka Magufuli.
Wakati tukiendelea kuungana na serikali, watu binafsi na wadau mbalimbali kumkumbuka leo Magufuli kwa mema aliyoifanyia nchi, vilevile tunatambua na kumpongeza Rais wa Awamu ya Sita, Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza gurudumu bila kutetereka.
Rais Samia ambaye aliapishwa kuongoza nchi Machi 19, 2021, ikiwa ni siku mbili baada ya kifo cha Magufuli, pia ni sehemu ya maendeleo wakati wa Serikali ya Awamu ya Tano kwani ndiye alikuwa Makamu wa Rais.
Tunampongeza kwa juhudi za kuendeleza maendeleo ya mtangulizi wake kiasi cha kuleta faraja na matumaini makubwa kwa Watanzania.
Isitoshe, Rais Samia amekuja na mambo mengine mapya na makubwa yanayoimarisha ustawi wa nchi na kila Mtanzania.
Rais Samia ameonesha umahiri katika kuleta mafanikio katika sekta za afya, elimu na uchumi kwa ujumla.
Uongozi wa Rais Samia umejikita pia katika kujenga umoja na mshikamano kati ya wananchi, huku akisisitiza umuhimu wa usimamizi mzuri wa rasilimali za taifa.
Ameongoza bila kutetereka huku akiimarisha uhusiano wa kidiplomasia na mataifa mengine, huku akichangia katika juhudi za kuleta amani na utulivu katika Kanda ya Afrika Mashariki.
Amejenga mazingira bora ya biashara, amevutia wawekezaji wengi jambo ambalo linatia nguvu uchumi wa Tanzania.
Ni wazi kwamba Watanzania tunamkumbuka Magufuli chini ya falsafa yake ya ‘Hapa Kazi tu’ ambayo iliidhihirisha; lakini tukiwa na faraja na matumaini makubwa kutokana na uendelevu wa uchapa kazi chini ya Rais Samia.
Hakika Rais Samia chini ya falsafa yake ya ‘Kazi Iendelee’ ameitendea haki safari ya maendeleo ya Tanzania aliyoianzisha Magufuli wakati wa awamu ya tano.
Tunamtakia kila heri Samia na kuitakia nchi yetu ufanisi na mustakabali bora zaidi wa amani, upendo na utulivu kama ambavyo serikali yake imejizatiti kuyaendeleza.
Aidha, tunakumbusha umma wa Watanzania na viongozi kwa ujumla, kuzingatia utamaduni wa kurithi fikra na maono mema ya watangulizi kwa mustakabali mwema wa kizazi kijacho tukihimiza ‘Kazi Iendelee’. Hongera Rais Samia kwa kuenzi mema yote ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Get a press release about habarileo.co.tz featured on major news sites GUARANTEED! See how it’s done: bit.ly/prpress
AI is Rewriting Search—Will You Still Be Found? Traditional SEO isn’t enough anymore. AI and voice search are already controlling half of all searches, and if your site isn’t prepared, your rankings could disappear overnight.
I can help make sure your business stays ahead. Let’s do a free audit—email me at Admin@Marketer2025.com or visit Marketer2025.com before it’s too late.
Hit them back
https://www.speed-seo.net/product/negative-seo-service/
whatsapp: +1 (833) 454-8622
Hi ,
I came across habarileo.co.tz today and was genuinely impressed by your work and audience engagement. on thus oage Mayeye afungua pazia mbio za uenyekiti ACT Kigoma – HabariLeo I also Just found, https://zaya.io/08559 this cool software that I thought you might like. It makes creating viral video super easy and publishes it automatically everywhere.
The best part? It does all the heavy lifting while you just oversee things. And the money it brings in is pretty sweet! I’ve been using it myself and loving the results.
Get habarileo.co.tz featured on major news sites GUARANTEED! Attract high-value customers and outperform your competitors. See how it’s done: bit.ly/prpress